ENTERTAIMENTS

Pinda kubariki Tamasha la Pasaka Dar


Waziri Mkuu Mizengo Pinda
Waziri Mkuu Mizengo Pinda anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika Tamasha la Pasaka litakalofanyika Machi 31 kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Taarifa kwa vyombo vya habari, iliyotolewa jana na mwenyekiti wa kamati ya maandalizi ya tamasha hilo, Alex Msama, ilieleza kuwa tayari Ofisi ya Waziri Mkuu imethibitisha kuhusiana na ujio wake kwenye tamasha hilo.
“Tunafurahi kwamba katika tamasha letu mwaka huu jijini Dar es Salaam, mgeni rasmi atakuwa Waziri Mkuu Mizengo Pinda... mwaka jana alikuwa Waziri wa Mambo ya Nje, Benard Membe,” ilisema sehemu ya taarifa hiyo.
Waimbaji mbalimbali wa ndani na nje ya Tanzania wanatarajiwa kutumbuiza katika tamasha hilo, ambapo wasanii wa nje ya nchi ni Ephraim Sekeleti wa Zambia, Sipho Makhabane wa Afrika Kusini na Solomon Mukubwa raia wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo anayeishi Kenya, pamoja na kwaya ya Ambassadors of Christ ya Kigali nchini Rwanda.
Waandaajia wamewataja wasanii wenyeji watakaotumbuiza wakati wote wa tamasha hilo kuwa ni Upendo Kilahiro,  Rose Muhando, Upendo Nkone na John Lissu. Makundi ya kwaya ya Kinondoni Revival na Glorious Celebration pia yatakuwapo.


Azam walk on tight rope


Azam FC squad
Azam walk on tight rope as any slip up in their remaining three matches could easily hand over the Mainland premiership title to pacemakers Young Africans.

The team needs to perfect and win the rest of the fixtures while praying for Yanga to stagnate at the 56-point mark, Azam’s maximum ceiling.

The ice-cream makers are nine points adrift of champions to be Yanga and meet Coastal Union on April 26 at the Mkwakwani Stadium in Tanga.

The Dar side is the only team which has the probability of attaining the mark already touched by Yanga after Sunday’s 3-0 wig over relegation-haunted JKT Ruvu.
Any other result other than victory for the ice-cream makers would automatically shatter their title chasing dreams for the season they fought gallantly to lift it.

Azam were not in action over the weekend following their CAF Confederation Cup commitment as they faced visiting Moroccan side AS Far to salvage barren draw.

Yanga need to win or at least pull a draw in one of their two remaining fixtures one against Coastal Union and the other versus dethroned champions Simba on May 18.

Miss Tabata 2013 kupatikana Mei 31

Warembo wakiwa mazoezini.
Shindano la kumsaka mrembo wa Tabata, Miss Tabata 2013, litafanyika Mei 31 katika ukumbi wa Da’ West Park, Tabata, waandaaji wamesema.

Mratibu wa shindano hilo, Joseph Kapinga amesema kuwa shindano hilo litakuwa ni la aina yake kulinganisha na mashindano ya miaka ya nyuma kwani mwaka huu wamemejitokeza warembo wazuri zaidi.

“Warembo wazuri zaidi wamejitokeza mwaka huu kuliko mashindano tuliyowahi kuyafanya nyuma. Tutakuwa na burudani nyingi kutoka nje na ndani ya nchi,” alisema mratibu huyo wa Bob Entertainment na Keen Arts.

Warembo watakaoshiriki kwenye shindano wanaendelea na mazoezi kila siku katika ukumbi wa Da’ West Park.

Warembo hao ni Pendo Moshi (20), Madgalena Bhoke (21), Kabula Kibogoti (20), Queen Masha (19), Upendo Dickson (22), Martha Gewe (19), Zilpha Christopher (19), Hidaya David (22), Aneth Ndumbalo (19), Amina Ally (18), Dorice Mollel (22), Eunice Nkoha (19), Kazunde Kitereja (19),  Angela Fradius (19), Domina Soka (21), Rehema Kihinja (20), Glory Jigge (18) na Sophia Claud (21).

No comments:

Post a Comment