Kikwete aanza ziara mkoani Morogoro

Rais Jakaya Kikwete
Akiwa mkoani humu, Rais Kikwwete atatembelea Chuo Kikuu cha Waislamu (MUM) na kuendesha harambee ya ujenzi wa Kanisa Katoliki la Kigurunyembe la Jimbo Katoliki la Morogoro.
Harambee hiyo itafanyika katika bwalo la Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), Magadu, mjini hapa.
Kwa mujibu waa Afisa Uhusiano wa MUM, Ally Saddy, Rais Kikwete ambaye aliwasili mkoani humu jana, leo asubuhi ataweka jiwe la msingi katika jengo la Teknolojia ya Habari na Mawasiliano ICT la chuo hicho.
Kadhalika, alisema Rais Kikwete atafungua jengo la kitivo cha sayansi na baadaye atazungumza na jumuiya ya wanachuo na wananachi wa Mkoa wa Morogoro.
Kwa upande wake, Katibu wa Jimbo Katoliki Morogoro, Padri Luitfrid Makseyo, alisema Rais Kikwete ataendesha harambee ya ujenzi wa Kanisa la Parokia ya Kigurunyembe.
Padri Makseyo alisema jengo hilo mpaka sasa tayari limegharimu Sh. milioni 130.
Alisema lengo la harambee hiyo ni kupata Sh. milioni 200 ili kuendelea na ujenzi wa hatua za awali na hadi kukamilika kwake litagharimu Sh. milioni 600.
Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Joel Bendera, aliwataka wakazi wa mkoa huo kujitokeza kwa wingi kwenye viwanja vya Chuo Kikuu cha Kiislamu ili kumsikiliza Rais Kikwete wakati wa mkutano huo wa hadhara.
Aliwataka kutambua kuwa ujio wake mkoani Morogoro ni heshima kubwa na kuwaomba wananachi kujitokeza kwenye hara
Conservatives Spar over Economics of Immigration Reform
Co-author of the Heritage study Robert Rector and American Action Forum's Douglas Holtz-Eakin faced-off on the economics behind the immigration bill on CNBC's "The Kudlow Report" Monday night.
No comments:
Post a Comment